JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Ulinzi Blog

Matukio Mbalimbali

Naibu Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Dkt Asharose Migiro akiwasili Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es Salaam alipomtembelea Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Davis Mwamunyange kulia ni Kanali Adolph Muta

 

Dkt Asharose Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manungi, kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

 

Mkuu wa Msafara wa Ujumbe kutoka Jeshi la Anga la Marekani akisalimiana na Kamishina wa Idara  ya Maendeleo ya Jeshi na Utafiti Brigedia Jenerali Kelvin Msemwa mara baada ya kumaliza kikao Msasani Beach Club.

 

Pichani ni Ujumbe wa Msafara kutoka Jeshi la Anga la Marekani na wenyeji wao hapa nchini wakiwa Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam.

Posted on 03-Aug-12 18:35.


Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Kikundi cha bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa kikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Posted on 15-Sep-11 12:24.


Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Posted on 15-Sep-11 12:19.


Sherehe ya kuwaaga Maafisa Wakuu wastaafu wa JWTZ

Maafisa Wakuu Jeshini wakisukuma gari lililowabeba Maafisa Wakuu wastaafu wa JWTZ Meja Jenerali Yodan Kohi (kushoto) ambaye alikuwa Mkuu wa Huduma ya Tiba  Makao Makuu ya Jeshi na Meja Jenerali Salim Salim (kulia) ambaye alikuwa Mkuu wa Hospitali Kuu ya Kijeshi Lugalo.

Posted on 18-Aug-11 06:54.


Maafisa na Askari 73 wa JWTZ wahitimu mafunzo ya udereva ngazi ya cheti katika Chuo cha VETA

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. James Msekela (watatu kutoka kushoto waliokaa kwenye viti) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari 73 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kanda ya Dodoma waliohitimu mafunzo ya udereva ngazi ya cheti katika chuo cha VETA mjini Dodoma. (Picha na Sajenti Joel Mjengi, Dodoma)

Posted on 10-Aug-11 13:53.


Sherehe za maadhimisho ya siku ya Mashujaa iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam tarehe 25 Jul 2012

Baadhi ya wazee waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakifatilia kwa umakini matangazo kabla kuanza maadhimisho ya Siku ya Mashujaa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Kikundi cha Askari wa Jeshi la Nchi Kavu na Jeshi la Kujenga Taifa kikiwa kimesimama kwa ukakamavu siku ya Mashujaa.

Kikundi cha Askari cha Maombolezo kikitoa heshima katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa siku ya maadhimisho hayo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akiweka Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Adolf Mwamunyange akiweka Sime kwenye Mnara.

Kiongozi wa Mabalozi, Balozi wa DRC nchini Mhe. Khalfan Mpango akiweka shada la maua kwenye Mnara.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt Didas Masaburi akiweka upinde na msahale.

Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam, Mzee Rashidi Ngonja akiweka shoka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dkt Omari Ali Juma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha akihutubia wageni waalikwa(hawapo pichani) katika tafrija ya kuadhimisha siku ya Mashujaa

iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu (kushoto) akitembea kwenda kuweka Ngao na Mkuki kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa mjini Songea.
Posted on 27-Jul-11 13:26.


Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini China

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa ajili ya mapokezi yake rasmi alipofanya ziara nchini humo hivi karibuni, kulia kwake ni Mkuu wa Jeshi hilo Jenerali Chen Bingde.

Posted on 04-Jul-11 08:28.


Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini China

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa kwenye mazungumzo rasmi nchini China na Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Chen Bingde hivi karibuni.

Posted on 02-Jul-11 20:40.


Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini China

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na ujumbe wake wakiwa na Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China na Makamanda wa ngazi za juu wa Jeshi hilo alipofanya ziara yake nchini humo hivi karibuni.

Posted on 02-Jul-11 20:36.


Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini China

Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa ziara yake ya kikazi nchini China hivi karibuni akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi wa China Jenerali Liang Guanglie ambaye pia ni State Councilor nchini humo (wa tano kutoka kulia mbele) na wanne kutoka kulia mbele ni Balozi wa Tanzania nchini humo Mheshimiwa Omari Mapuri.

 

Posted on 02-Jul-11 20:28.


Semina Elekezi iliyofanyika mjini Dodoma

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina elekezi mjini Dodoma

Posted on 24-May-11 09:47.


Sherehe za Miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiingia katika uwanja wa Amaan mjini Unguja kuadhimisha sherehe za miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 

Posted on 01-May-11 19:22.


Yaliyoandikwa kwenye hii ULINZI Blog hayakusudii kuwasilisha sera, mtazamo na maoni ya uongozi wa Jeshi.