• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

GAFTAG NA JWTZ KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA MASWALA YA UTAFITI WA ULINZI WA AMANI

GAFTAG NA JWTZ KUIMARISHA USHIRIKIANO  KATIKA MASWALA YA UTAFITI WA ULINZI WA AMANI Posted On: Thursday, 3rd March 2022

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo March 3, 2022 limekabidhiwa Jengo la Utafiti na Kikundi cha Ushauri wa Kiufundi Cha Jeshi la Ujerumani (German Armed Forces Technical Advisory Group - GAFTAG) lililojengwa katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam. Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti (United National Institute of Training and Research – UNITAR).

Makabidhiano hayo yamefanyika kati ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Mathew Mkingule ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti Claudia Cnoci ambaye amemuwakilisha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Kathrin Steinbrenner.

Kupatikana kwa Jengo hilo kutasaidia kuboresha mafunzo na utafiti katika Kituo Cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani. Aidha, Maafisa na Askari watakaopata mafunzo kituoni hapo watanufaika kwa kupata ujuzi zaidi kabla ya kwenda kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani watakapopangiwa. Vile vile mafunzo hayo yatawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi na weledi.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.