Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujeng Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax Leo Tarehe 29 September, 2025 ameweka jiwe la Msingi katika Kiwanda cha kuzalisha Magari ya Kijeshi utakaofanywa kwa ubia kati ya Kampuni ya Streit Group toka Falme za Kiarabu(UAE) na Shirika la TATC Nyumbu Kibaha Pwani.
Soma zaidiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 27 Septemba, 2025 amemkabidhi Sajini taji Alphonce Simbu zawadi ya nyumba baada ya kushinda kwenye mashindano ya mbio za Dunia kwa umbali wa kilomita 42 zilizofanyika nchini Japan.
Soma zaidiMshindi wa medali ya dhahabu katika Mashindano ya Marathoni ya Dunia yaliyofanyika Tokyo Japan Sajini Alphonce Simbu amepokelewa kishujaa na Serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jijini Dar es Salaam.
Soma zaidiTimu za Ngome zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania zimezidi kung'ara katika mashindano ya Michezo mbalimbali ya Majeshi (BAMMATA) ambayo yanafanyika mjini Zanzibar.
Soma zaidiMkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda leo tarehe 12 Septemba 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Polisi Jeshi katika kijiji cha Mkanzaule Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa.
Soma zaidiRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua Mashindano ya Michezo ya Majeshi BAMMATA kwa mwaka wa 2025, ambayo yanafanyika mjini Zanzibar.
Soma zaidiMkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa nchi za Falme za Kiarabu, Luteni Jenerali Eisa Saif Mohamed Bin Ablan Almazrouei amefanya ziara ya kikazi nchini Tanzania leo tarehe 14 Julai 2025.
Soma zaidiJeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetoa msaada wa maboksi mia moja ya vigae na matenki matano yenye ujazo wa lita elfu kumi kila moja kama mchango wake katika ujenzi wa nyumba nane zilizopo Wilaya ya Karongi nchini Rwanda, kwaajili ya manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Soma zaidiTanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.