Posted On: Monday, 3rd November 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha pili katika sherehe zilizofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba 2025.
Akilihutubia taifa mara baada ya kula kiapo, Rais Dkt. Samia amewashukuru watanzania kwa kumchagua kuiongoza Tanzania kwa kipindi kingine na kusisitiza wananchi wote kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa na kuungana ili kulijenga taifa.
Aidha, Rais Samia amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa na shughuli za kila siku za wananchi kurejea baada ya vurugu zilizotokea wakati wa uchanguzi Mkuu na kusababisha uharibifu wa mali za umma na za watu binafsi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.