Posted On: Sunday, 23rd November 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatunuku kamisheni Maafisa 296 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Katika sherehe iliyofanyika katika Chuo cha Kijeshi Monduli mkoani Arusha tarehe 22 Novemba 2025.
Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Jackson Jairos Mwaseba amesema Maafisa hao wapya waliotunukiwa kamisheni wamehudhuria Mafunzo hapa nchini na kwenye Vyuo vya Kijeshi katika mataifa rafiki. Meja Jenerali Mwaseba alisema kuwa katika kundi hilo, Maafisa 39 ni wanawake na 257 ni wanaume.
Aidha, kati ya Maafisa 296 waliotunukiwa kamisheni, Maafisa 23 wanatoka mataifa ya Burundi, Comoro, Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Uganda na Zambia. Maafisa 89 ni watanzania ambao walifanya mafunzo katika nchi rafiki.
Mbali na kutunuku kamisheni Mhe. Rais aliwatunuku Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi Maafisa 106.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.