Posted On: Friday, 5th June 2026
Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Said idd Nkambi, amefungua kikao kazi cha Polisi Jeshi kinachofanyika katika Kikosi cha Mazao Mkoani Morogoro tarehe 04 Jun 26.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Meja Jenerali Nkambi amewaasa Polisi Jeshi kutumia fursa ya kikao hicho kujadili namna nzuri ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuleta tija katika utendaji wa Polisi Jeshi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na hivyo kuliletea Jeshi sifa nzuri.
Sambamba na hilo amewataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria mbalimbali na mabadiliko yake ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
Kikao kazi hiki kinachoongozwa na Mkurugenzi wa Polisi Jeshi Brigedia Jenerali Abubakar Charo ni mwendelezo wa vikao vinavyofanyika kila mwaka katika kamandi mbalimbali ambapo mwaka huu Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi imepewa dhamana ya kuandaa Kikao kazi hicho. Hiki ni kikao kazi cha Saba tangu kuanzishwa kwa vikao kazi vya Kurugenzi ya Polisi Jeshi.
Washiriki wa Kikao ni Maafisa wanadhimu kutoka Kurugenzi ya Polisi Jeshi Makao Makuu ya Jeshi, Kurugenzi ya Polisi Jeshi Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, Wakuu wa Polisi Jeshi wa Kamandi, Brigedi na Shule za Mafunzo ya Kijeshi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.