• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Jenerali Mabeyo atembelea Mafunzo ya Makocha

Jenerali Mabeyo atembelea Mafunzo ya Makocha Posted On: Wednesday, 12th June 2019

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo ametembelea mafunzo ya Makocha wa Mpira wa Kikapu, Ngumi na Waamuzi wa Mpira wa Kikapu.

Katika ziara hiyo Jenerali Mabeyo alianza kwa kuangalia mafunzo yaMchezo wa Kikapu yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari JitegemeeMgulani na kuendelea kwa kukagua darasa la Waamuzi wa Mpira wa Kikapu.

Aidha, akiwa katika viunga vya Mgulani alipata nafasi ya kuangalia mafunzo ya Makocha wa Ngumi wakiwa katika mafunzo kwa vitendo pale walipokuwa wakiwafundisha Vijana wa Timu ya Ngumi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Ukumbi wa Mabatini uliopo JKT Mgulani.

Akiwa Ukumbini hapo aliongea na Washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia mafunzo ili yalete tija kwa Jeshi na Taifa kwa ujumla.

“Zingatieni mafunzo mnayoyapata hapa ili na nyinyi muende mkawafikishie wenzenu huko mnakotoka kwani kwa kufanya hivyo Majeshi yetu yatakuwa na Timu bora na kuendeleza sifa iliyojengeka kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya vizuri katika Sekta hii ya Michezo” alisema Jenerali Mabeyo.

Vilevile aliipongeza Kurugenzi ya Michezo Jeshinikupitia mwakilishi wetu aliyeko kwenye Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani Kanali Joseph Bakar kwa kutuletea Wakufunzi kutoka Ujerumani kwa ajili ya kuwapatia elimu zaidi Makocha wetu hapa nchi kwa maslahi ya nchi.

Hata hivyo alimtaka afanye utaratibu wa kuwaleta Wakufunzi kwa upande wa Michezo mingine ikiwemo Mpira wa Miguu na waje kwa Mafunzo ya muda Mrefu ikiwezekana hata mwaka mmoja ili timu zetu ziendelee kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

“Wakati mwingine utuletee Makocha wa Mpira wa Miguu kwa ajili ya Timu za Jeshi ili ziweze kufanya vizuri kitaifa na Kimataifa” alisema Jenerali Mabeyo

Mafunzo haya ni mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika mwaka jana yenyelengo la kuwaongezea ujuzi zaidi Makocha wetu wa michezo hiyo ili kuendele kuvifanya vyombo vya Ulinzi na Usalama viewe sehemu pekee ya kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo mbalimbali hapa nchini kupitia vituo vya michezo hiyo kote nchini na kutengeneza ajira kwa wale wanaopata nafasi ya kujiunga na Timu mbalimbali.

Jumla ya washiriki sitini na tatu (63), Wanaume idadi Hamsini (50) na Wanawake kumi na watatu (13) kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wamehudhuria mafunzo hayo ya wiki mbili.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.