• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

​Jenerali Mkunda ahitimisha zoezi la uvishaji Nishani

​Jenerali Mkunda ahitimisha zoezi la uvishaji Nishani Posted On: Friday, 28th March 2025

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda amehitimisha zoezi la uvishaji nishani kwa kuwavisha Nishani mbalimbali Maafisa na Askari wa JWTZ Kanda ya Mtwara leo tarehe 28 Machi 2025.

Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Shughuli za Rais,Sura ya 9,Toleo la Urekebu la mwaka 2002 alitunuku nishani mbalimbali ambapo Jenerali Mkunda amevalisha nishani hizo kwa niaba yake.

Miongoni mwa waliovishwa nishani hizo leo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Michael Mangwela Mntenjele .

Akizungumza baada ya kuvisha nishani hizo, Jenerali Mkunda amewapongeza Maafisa na Askari waliotunukiwa nishani hizo kwa namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan alivyotambua mchango wao katika kulitumikia Taifa kwenye nyanja ya Ulinzi.

Aidha,amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi yetu inakuwa salama wakati wote.

Nishani hizo ni

Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema,Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ na Nishani ya Jumuiya ya SADC.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.