• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Jenerali Mkunda awapongeza Maafisa na Askari

Jenerali Mkunda awapongeza Maafisa na Askari Posted On: Friday, 28th February 2025

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali, Maafisa na Askari wa JWTZ Kanda ya Songea tarehe 28 Februari 2025.

Miongoni mwa waliovishwa nishani ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ambaye ametunukiwa Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Miaka 60 ya Muungano na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.

Akizungumza baada ya kuwavisha nishani, Jenerali Mkunda amewapongeza Maafisa na Askari waliotunukiwa nishani hizo kwa kumshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyotambua mchango wao katika kulitumikia taifa kwenye nyanja ya ulinzi.

Jenerali Mkunda amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi yetu inakua shwari na salama wakati wote.

Nishani walizotunukiwa ni pamoja na Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, Nishani ya Miaka 60 ya Muungano, Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Nishani ya Ulinzi wa Amani ya Jumuiya ya SADC.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.