• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

JWTZ laanza rasmi kutekeleza agizo la Amiri Jeshi Mkuu

JWTZ laanza rasmi kutekeleza agizo la Amiri Jeshi Mkuu Posted On: Wednesday, 14th November 2018

Hatimaye malori ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yameanza rasmi safari ya kuelekea mikoa ya Kusini na Pwani katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli la kusomba korosho na kuzipeleka katika maghala yaliyoteuliwa na Serikali.

Akizungumza na Madereva Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Meja Gaudence Ilonda amesema, JWTZ linaendelea na operesheni hiyo ambayo haitakuwa na athari yoyote kwa wananchi ambao wapo maeneo hayo kwa kuwa hii si Operesheni ya Kijeshi bali tunaenda kusaidia wananchi.

Aidha, Magari mengine yanaendelea kuondoka ili kutekeleza operesheni hiyo kwa weledi mkubwa na kwa muda muafaka, ambapo zaidi ya magari 70 yanategemewa kufika mikoa ya kusini na Pwani kwa ajili ya kusomba korosho kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Tawi la Uhandisi na Ugavi Brigedia Jenerali Paul Simuli amesema kuwa magari yapo ya kutosha ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa. Pamoja na hayo amewaasa madereva kufanyakazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni ili kuhakikisha operesheni inakamilika kwa wakati.

Habari Mpya

  • Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa afungua mashindano ya CDF CUP.

    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa afungua mashindano ya CDF CUP.

    tokea siku 1
  • ​MEJA JENERALI GAGUTI AHITIMISHA MAFUNZO ASKARI WAPYA.

    ​MEJA JENERALI GAGUTI AHITIMISHA MAFUNZO ASKARI WAPYA.

    tokea siku 5
  • Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    tokea wiki 3
  • Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.