• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

JWTZ latumia ATCL kwenda Darfur Sudan

JWTZ  latumia ATCL kwenda Darfur Sudan Posted On: Friday, 17th May 2019

Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya Serikali ya ATCL ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli katika kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga amesema Jeshi ni Taasisi inayoongozwa na Uzalendo,uadilifu, uhodari hivyo ni faraja kubwa kwa Jeshina wapiganaji kuunga mkono jitihada za Serikali katika Kuboresha Uchumi ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuonesha uzalendo kwa vitendo kwa kutumia vitu vya nyumbani kwa maslahi mapana ya Taifa.

“ Tumekuwa tukitumia Ndege zetu za Jeshi lakini tumekuwa tukitumia Ndege za mataifa mengine kwa Mikataba kutoka Umoja wa Mataifa lakini sasa ni faraja kwani tumefanikiwa kuwashawishi Umoja wa Mataifa kutumia Ndege zetu” Alisema Meja Jenerali Kapinga.

Aidha,Meja Jenerali kapinga alisema mbali na kutumia Ndege hiyo lakini aliwaasa Maafisa na Askari hao kuhakikisha wanapeperusha vema Bendera ya Nchi na kuendelea kuitangaza kwa sifa nzuri za Utendaji Kimataifa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la la Tanzania (ATCL),Mhandisi Ladislaus Matindi alisema ni Fursa Nzuri kwa ATCL na wanalishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia kwa mkuu wa majeshi ya Ulinzikwa Mchango mkubwa kufanikisha kupata tenda hiyo.

“ Namshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na watendaji wake kwa Uzalendo wake na kuhakikisha anafanikisha ATCL kupata fursa kwa mara ya kwanza na hii itakuwa mwanzo mzuri na tutahakikisha tunaitumia vizuri fursa hii kujitangaza zaidi Kimataifa kwa maslahi ya Nchi “ Alisema Mhandisi Matindi.

Vilevile Mhandisi Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12 bila kusimama, hivyo kwa kutumia saa tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.

Naye Kamanda wa Kikosi cha TANZBATT- 13, Luteni Kanali Khalfan Kayage anayekwenda na Kikosi hicho alisema kuwa inawapa nguvu kupeperusha Bendera yetu kupitia Ndege na ameahidi kufanya kazi kwa Bidii kuendeleza jina na sifa nzuri ya Tanzania Kimataifa.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.