• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Kwaheri Dkt John Pombe Magufuli

Kwaheri Dkt John Pombe Magufuli Posted On: Friday, 26th March 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza maelfu ya waombolezaji kwenye mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika makaburi ya familia nyumbani kwake wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita.

Mazishi hayo yalitanguliwa na Misa maalum iliyofanyika Kanisani nyumbani kwake na baadae mwili kupelekwa katikauwanja wa Magufuli ambapo viongozi mbalimbali walitoa salaam za rambirambi akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan.Katika salaam hizo Mhe. Rais ameahidi kuendelea kutekeleza ilani yaCCM ili kuendeleza kasi ya maendeleo iliyoanzishwa na Hayati Magufuli.

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amesema kuwa hali ya usalama wa nchi na mipaka yake iko shwari, na pia Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wapo tayari kutii na kutoa ushirikiano mzuri kwa Mhe. Rais.

Mara baada ya kukamilika kwa ibada na salamu za rambirambi,mazishi yalifanyika nyumbani kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye eneo maalum lililoandaliwa ambapo taratibu za mazishi ya Kidini zilianzia na kuhitimishwa na mazishi ya kijeshi,ikiwemo kupigiwa mizinga 21ikiwa ni heshima ya juu kama ishara ya kumuaga kwa kutambua na kuthamini uongozi wake kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Shughuli hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Dinipamoja naviongozi wastaafu wakiwemo Mzee Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.