• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

​Meja Jenerali Nondo ahitimisha Zoezi PIMA UWEZO 2025

​Meja Jenerali Nondo ahitimisha Zoezi PIMA UWEZO 2025 Posted On: Thursday, 17th April 2025

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Brigedi ya Faru limehitimisha zoezi la medani PIMA UWEZO 2025 lillofanyika Mkoani Shinyanga.

Akimwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda katika kilele cha kuhitimisha zoezi hilo,Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu Meja Jenerali Fadhili Omary Nondo amewataka Maafisa na Askari kuwa tayari nyakati zote kulinda mipaka ya aridhini,angani na kwenye maji dhidi ya uvamizi wa adui.

" Mazoezi ni sehemu ya kutufanya Wanajeshi tuwe tayari nyakati zote katika kutekeleza majukumu ya ulinzi wa Taifa ,hivyo wakati wa amani tunapaswa kuvuja jasho jingi ili wakati wa Vita tutekeleze majukumu yetu kwa ufanisi mkubwa"

Aidha amesema mazoezi haya yataendelea kufanyika kwa nyakati na sehemu tofauti nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa na Askari wa JWTZ.

Kwa upande wake Kamanda wa Brigedi ya Faru Brigedia Jenerali Gabriel Elias Kwiligwa amesema zoezi hili limefanyika kwa siku 12 likiwa na lengo la kupima utayari wa vikundi katika kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo ugaidi, uvamizi wa vikundi kutoka ndani na nje ya nchi na kuzuia uhamiaji haramu.

Zoezi la Medani PIMA UWEZO 2025 lenye kauli mbiu isemayo" PIMA UWEZO,KAA TAYARI TUILINDE TANZANIA" lililofanyika Mkoani Shinyanga pia limeshirikisha Askari wa Jeshi la Akiba(Mgambo).

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.