• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Mkuu wa Majeshi ya Msumbiji atembelez Tanzania

Mkuu wa Majeshi ya Msumbiji atembelez Tanzania Posted On: Tuesday, 6th September 2022

Mkuu wa Majeshi ya Msumbiji Admiral Joaquin Rivas Mangrasse amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda wakati wa ziara yake ya kikazi hapa nchini.

Mara baada ya kuwasili, Mkuu wa Majeshi ya Msumbiji alikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Aidha, Mkuu huyo wa Majeshi alipata fursa ya kusalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax.

Ziara hiyo inalenga kuongeza ushirikiano wa kijeshi baina ya Tanzania na Msumbiji ili kuboresha na kuimarisha ulinzi na usalama baina ya nchi hizi mbili.

Katika mazungumzo yao wakuu hao wa Majeshi wamesema usalama wa nchi hizi utachangia maendeleo ya wananchi wake.

Ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji umedumu kwa muda mrefu tangu enzi za waasisi wa mataifa haya Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Samora Machel wa Msumbiji.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.