• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Rais Samia Suluhu Hassan aongoza maelfu kumuaga Dkt. Magufuli

Rais Samia Suluhu Hassan aongoza maelfu kumuaga Dkt. Magufuli Posted On: Saturday, 20th March 2021

Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 20 Machi 2021 amewaongoza Viongozi na maelfu ya Watanzania katika shughuli za kutoa Heshima za Mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli katika Kiwanja cha Uhuru jijini Dar es Salaam.

Shughuli hizo za kuuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli zilianza majira ya saa tatu asubuhi baada ya sala iliyofanyika uwanjani hapo iliyoongozwa na Baba Askofu Mkuu Rua'ich wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Awali Mwili wa Hayati Dkt. Magufuli ulifanyiwa Misa maalum katika Kanisa la Mtakatifu Peter, Oysterby kabla ya kufikishwa uwanjani hapo.

Aidha, shughuli za kuaga zitaendelea tena tarehe 21 Machi 2021 katika Kiwanja hicho kwa wananchi waishio mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani kupewa fursa ya kutoa Heshima za Mwisho kwa mwili wa mpendwa wao Hayati Dkt. John Pombe Magufuli..

Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Viongozi wa kidini na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo walishiriki kuuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli..

Wakati wa shughuli hizo vilio, simanzi na majonzi vilitawala kiwanjani hapo na hata baadhi ya wananchi kuzimia kwa kuonesha mapenzi ya dhati kwa kiongozi wao.

Siku hiyo ya kwanza zoezi hilo la kuaga lilikamilika majira ya saa mbilii usiku. Siku ya Jumatatu mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli utapelekwa Makao Makuu ya nchi Jijini Dodoma kwa ajili ya kuwapa fursa wakazi wa jiji hilo kutoa Heshima zao za mwisho kabla ya kupelekwa Zanzibar siku inayofuata na baadae kupelekwa jijini Mwanza na hatimae Mkoani Geita kupewa Heshima za Mwisho. Mwili wa kipenzi cha Watanzania, Dkt. John Pombe Magufuli unatarajiwa kuzikwa rasmi tarehe 26 Machi,2021 Kijijini kwake Chato, Mkoani Geita.

Hayati Dkt. Magufuli atakumbukwa kwa uongozi wake makini, kupambana na rushwa, kujenga taasisi yenye utamaduni wa kuchapa kazi kupitia falsafa yake ya "Hapa Kazi tu", kuyahamishia Makao Makuu ya nchi Mkoani Dodoma, kujenga miundombinu ya afya na elimu nchini kote, kutoa elimu bila Watanzania kulipia kuanzia shule ya Msingi hadi kidato cha nne, kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kufikisha umeme takriban vijiji 10,000 kati 12,000 nchini, ujenzi wa Kijazi Interchange na Mfugale Flyover Mkoani Dar es Salaam, ujenzi wa Madaraja ya Tanzanite pale Salender Bridge Dar es Salaam na Kigongo Busisi linalounganisha Mikoa ya Mwanza na Geita, ujenzi wa Meli katika Maziwa yote Makuu nchini, upanuzi wa barabara na madaraja nchini kote sambamba na kuanzisha miradi ya kimkakati ya SGR, Mradi wa Bwawa la Umeme la Nyerere, na kufufua ATCL.

Hayo machache ni mifano ya mafanikio makubwa yaliyotokana na nidhamu bora ya ukusanyaji wa kodi na matumizi sahihi ya kodi za Watanzania, kuimarisha uchumi wa viwanda na Uchumi wa Blue hadi kuiingiza Tanzania kwenye Uchumi wa Kati miaka mitano kabla ya malengo ya Ilani ya Chama alichokiongoza.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.