• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI Posted On: Wednesday, 30th April 2025

1.Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu. Aidha, uandikishaji utahusisha vijana wa Kitanzania wenye Taaluma Adimu.

2.Wataalamu hao watakaoandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali muhimu ya Kijeshi na mafunzo ya kuwaendeleza katika taaluma zao.

SIFA ZA MWOMBAJI

3.Vijana wa Kitanzania wenye nia ya kuandikishwa Jeshi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

a. Awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa. b Awe na afya nzuri na akili timamu,

c.Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa.

d.Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya Shule na vyeti vya Taaluma.

e.Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi cha Kuzuia Magendo.

f.Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea au Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.

g.Kwa vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita wawe na umri usiozidi miaka 24, Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya Juu umri usiozidi miaka 27 na Madaktari Bingwa wa Binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa.

4.Taaluma Adimu zinazohitajika ni ifuatavyo:-

a. Taaluma ya Tiba

(1) Medical Doctor (Specialist)

Generall Surgeon, Orthopaedic Surgeon, Urologist Radiologist, ENT Specialist, Anaesthesiologist, Physician,

Ophthalmologist, Paediatrician, Obstetrician & Gynaecologist, Ocologist, Pathologist, Psychiatrist, Emergency Medicine Specialist na Haematologist.

(2) Medical Doctor, Dental Doctor, Veterinary Medicine, Bio Medical Engineer, Dental Laboratory Technician, Anaesthetic, Radiographer, Optometry, Physiotherapy na Aviation Doctor.

b.Taaluma za Uhandisi (Engineer).

Bachelor of Electronic Engineering, Bachelor of Mechanical Engineering, Bachelor in Marine Engineering, Bachelor in

Merine transportation and Nautical Science, Bachelor in Mechanics in Merine Diesel Engine, Bachelor in Aviation Management, Bachelor in Aircraft Accident and Incident Investigation, Bachelor in Meteorology, Air Traffic Management na Aeronautic Engineering.

c.Fundi Mchundo.

Aluminium Welding na Welding and Metal Fabrication.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI KWA MAKUNDI YOTE MAWILI

5. Maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe Makao

Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 hadi tarahe 14 Mei, 2025 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:-

a.Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au nambari ya NIDA.

b.Nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya Shule na Chuo.

c.Nakala ya cheti cha JKT kwa waombaji waliomaliza mkataba wa kujitolea.

d.Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji.

MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO

Mkuu wa Utumishi Jeshini,

Makao Makuu ya Jeshi,

Sanduku la Posta 194,

DODOMA, Tanzania

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 1
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 1
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.