• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

TANZIA

TANZIA Posted On: Friday, 11th September 2020

TANZIA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anasikitika kutangaza vifo vya Maafisa wafuatao:-

Brigedia Jenerali Nelson Hosea Msanja (Mstaafu)

Kilichotokea tarehe 10 Setemba 2020 katika Hospitali ya Life Groenkloof nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu Brigedia Jenerali Msanja (Mstaafu) alizaliwa tarehe 01 Julai, 1958 katika Kijiji cha Utemini, Tarafa ya Utemini, Wilaya ya Singida, Mkoa wa Singida. Alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 19 Disemba 1979.

Katika utumishi wake Jeshini marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Kaimu Mkuu wa Tawi la Ukaguzi Jeshini (2013 – 2015); Kamishna wa Utafiti na Maendeleo ya Jeshi Wizara ya Ulinzi na JKT (2015 – 2017); Kaimu Mkuu wa Tawi la Uhandisi na Logistic Jeshini (2017) na Mwambata Jeshi nchini Afrika Kusini hadi alipostaafu kwa heshima tarehe30 Juni 2020.

Brigedia Jenerali Msanja (Mstaafu) alitunukiwa medali zifuatazo katika miaka 40 na miezi sita ya utumishi wake:-

Vita ya Kagera; Miaka 20 ya JWTZ; Utumishi mrefu; Miaka 40 ya JWTZ; Utumishi uliotukuka; Nishani ya Comoro; Miaka 50 ya Uhuru; Miaka 50 ya Muungano na Miaka 50 ya JWTZ.

Marehemu ameacha familia. Mipango ya mazishi inafanywa na Makao Makuu ya Jeshi kwa kushirikiana na familia.

Mungu ailaze roho ya marehemu Brigedia Jenerali Nelson Msanja (Mstaafu) mahali pema peponi – Amina.


Kanali James Robert Sarungi (Mstaafu)

Kilichotokea tarehe 11 Septemba 2020 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu Kanali James Robert Sarungi (Mstaafu) alizaliwa tarehe 01 Julai, 1955 katika Kijiji cha Utegi, Tarafa ya Utegi, Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara. Alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 17 Disemba 1973.

Katika Utumishi wake Jeshini marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi (1996 – 1998); Kaimu Mkuu wa Chuo Kunduchi Training Center (2006); Mshauri Jeshi la Akiba (2006) hadi kustaafu kwake 30 Juni 2013.

Marehemu Kanali James Robert Sarungi (Mstaafu) alitunukiwa medali zifuatazo katika miaka 39 na miezi sita ya utumishi wake:-

Vita ya Kagera; Miaka 20 ya JWTZ; Utumishi mrefu; Miaka 40 ya JWTZ; Utumishi uliotukuka; Nishani ya Comoro na miaka 50 ya Uhuru.

Marehemu ameacha familia. Mipango ya mazishi inafanywa na Makao Makuu ya Jeshi kwa kushirikiana na familia.

Mungu ailaze roho ya marehemu Kanali James Robert Sarungi (Mstaafu) mahali pema peponiAmina.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.