• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

TANZIA

TANZIA Posted On: Friday, 5th February 2021

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anasikitika kutangaza kifo cha Afisa Mkuu Brigedia Jenerali Ezra Wilson Ndimgwango (Mstaafu), kilichotokea tarehe 03 Februari 2021 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Marehemu alizaliwa tarehe 30 Desemba 1953 katika Kijiji cha Shunga, Kata ya Shunga, Tarafa ya Buhoro, Wilaya ya Kasulu katika Mkoa wa Kigoma. Alipata Elimu katika ngazi mbalimbali ikiwemo Project Management mwaka 2000 hadi 2001 nchini Tanzania na Conflict Management nchini Zimbabwe mwaka 2001.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 02 Mei 1974. Alihudhuria kozi mbalimbali ikiwemo kozi ya Afisa Mwanafunzi nchini Canada na kutunukiwa Kamisheni tarehe 01 Juni 1977. Marehemu alipandishwa vyeo ngazi kwa ngazi hadi cheo cha Brigedia Jenerali mnamo tarehe17 Septemba 2012. Marehemu alilitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 41 na miezi 9 hadi alipostaafu utumishi Jeshini kwa umri tarehe 31 Januari 2016.

Brigedia Jenerali Ezra Wilson Ndimgwango (Mstaafu) alitunukiwa Medali mbalimbali wakati wa utumishi wake ifuatavyo:- Medali ya vita; Miaka 20 ya JWTZ; Utumishi Mrefu; Miaka 40 ya JWTZ; Utumishi Uliotukuka; Miaka 50 ya JWTZ; Miaka 50 ya Muungano; Miaka 50 ya Uhuru na Nishani ya Comoro.

Katika utumishi wake Jeshini, Marehemu aliwahi kushika madaraka mbalimbali yakiwemo Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi la Anga mwaka 2009 hadi mwaka 2010 na Mkuu wa Kambi Kikosi cha Usafirishaji wa Anga mwaka 2012, madaraka aliyohudumu hadi anastaafu Jeshi kwa umri tarehe 31 Januari 2016.

Heshima za mwisho kwa marehemu zitatolewa Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 06 Februari 2021 kuanzia saa 03:00 asubuhi, na mazishi yatafanyika siku hiyo hiyo katika Makaburi ya ‘Air wing’ yaliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam. Marehemu ameacha mke na watoto.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.