• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

JWTZ latangaza nafasi kwa Madaktari

JWTZ latangaza nafasi kwa Madaktari Posted On: Sunday, 9th December 2018

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa JWTZ Meja Gaudence Ilonda amesema nafasi hizo zimetolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali, Vituo vya afya na Zahanati za Jeshi hilo kulingana na mahitajiya sasa na siku zijazo.

Aidha, watakaoandikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifuatazo; Daktari Bingwa wa Meno, Daktari Bingwa (Specialist Neurosurgeon), Mkemia, Mteknolojia Msaidizi (Assistant Laboratory Technician), Tabibu msaidizi(Assistant Clinical Officer), Katibu wa Hospitali, Msaidizi wa Kumbukumbu (Medical Records), Daktari (Medical Doctors),Afisa Muuguzi (Registered Nursing Officer), Fundi Sanifu vifaa tiba (Bio Medical Engineer), Tabibu (Clinical Assistant), Mfamasia (Pharmacist), Mtoa tiba kwa vitendo (Physiotherapist) na Afisa Muuguzi msaidizi.

Akifafanua zaidi Meja Ilonda amesema walengwa watakaoandikishwa jeshini ni wale wenye sifa zifuatazo:-

a.Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b.Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist.

c.Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.

d.Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri.

e.Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.

f.Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).

g.Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi.

h.Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

Meja Ilonda amewataka wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika Kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani Dar es Salaam tarehe 17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.

Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa usafiri, chakula na malazi.

Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayowaendeleza katika taaluma zao.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.