• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob John Mkunda awapongeza wanamichezo

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob John Mkunda awapongeza wanamichezo Posted On: Sunday, 6th April 2025

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kufanya vizuri katika michezo mbali mbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2025 .

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya Jeshi Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo leo hii wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpirawa magongo, na mpira wa kikapu.

" Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi wa Kimataifa kupitia Meja Mohamed Kasui kwa kuchaguliwa kuwa wa kwanza kutoka Afrika tangu mwaka 1948 kuwa Rais wa Kamati ya Kikapu ya Kijeshi Duniani jambo la kihistoria kwa Tanzania na Afrika".

Aidha, amesema kuwa Wanajeshi wamekuwa wakilitangaza Jeshi na Nchi Kitaifa na Kimataifa kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ambayo wamekuwa wakichaguliwa ama kuteuliwa kushiriki ndani na nje ya nchi.

" Michezo kwetu si burudani tu bali pia ni sehemu ya maandalizi ya Ulinzi wa Taifa, na hili ningependa iwe sehemu ya wajibu wa timu hizi au walezi wa michezo niliowateua ".

Naye Mkuu wa Operesheni na Utendaji Kivita Jeshini Meja Jenerali Ibrahim Mhona amesema kuwa wanamichezo wote waliofanikiwa wameonesha kuwa Askari wa JWTZ wanaweza kuwa shujaa ndani ya Uwanja wa Vita na Uwanja wa Michezo.

Wanamichezo waliofanya vizuri kimataifa ni pamoja na Praiveti King Lucas Mwajobaga ambaye ni Bingwa wa ngumi uzito wa Bantam Weight Afrika baada ya kumbwaga bingwa wa Angola yaliyofanyika Nchini Tunisia, Februari 2025.

Kwa upande wa mbio za Nyika timu ya wanaume waliibuka washindi wa kwanza katika mashindano ya Majeshi ya Dunia kipindi cha baridi (CISM Winter Games) Nchini Uswisi.

Timu ya Wanawake mbio za Nyika walishika nafasi ya tatu Machi 2025, huku praiveti Joseph Panga akishika nafasi ya pili kati ya wakimbiaji wa Mataifa zaidi ya 40.

Hafla hii ni kielelezo cha jinsi ambavyo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda anathamini nafasi ya michezo katika ujenzi wa Jeshi thabiti, lenye mshikamano na heshima.

Habari Mpya

  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 1
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 2
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 2
  • Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    Meja Jenerali Nkambi ateta na Ujumbe kutoka Jeshi la Uganda

    tokea wiki 2
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.