Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 17, 2018 amezindua Kituo cha Uwekezaji cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kilichopo katika Kambi ya Mgulani JKT Jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli amepata fursa ya kutembelea kiwanda cha maji ya Uhuru Peak na kiwanda cha ushonaji kituoni hapo.
Katika hotuba yake Dkt. Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na hatua ya JWTZ kuanzisha viwanda hivyo kwani vitaweza kupunguza tatizo la ajira pamoja na kulifanya jeshi kupunguza utegemezi.
Hafla fupi ya uzinduzi wa Kituo hicho cha Uwekezaji imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Utumishi Bora Mhe. George Mkuchika, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na viongozi wengine kutoka Serikalini na JWTZ.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.