Operation title

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea na jukumu la ulinzi wa amani nchini Lebanon chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa, mpango unaoitwa Jeshi la Mpito la Umoja wa Mataifa (United Nations Interim Force in Lebanon- UNIFIL ).

Tanzania ilipeleka kwa mara ya kwanza ya walinda amani mwezi Februari 2007. Walinda amani hao walipewa eneo kubwa la majukumu Kusini mwa Lebanon ambapo ilionekana kuwa ni changamoto kwa maafisa na askari kuhudumu eneo hilo .

Kutokana na ukubwa wa eneo hilo imeonekana kuna haja ya kuongeza nguvu, hivyo ilipofika mwaka 2011 eneo la Kusini mwa Lebanon likagawanywa katika sehemu kuu tatu ambazo ni UNIFIL HQ iliopo Naqoura, Sector West iliopo Shama na Sector East iliyopo Marjayoun.

Baada ya mgawanyo huo wa maeneo , JWTZ iliongezewa eneo lingine la ulinzi la Sector West hivyo kupelekea kuongeza Kombania ya pili katika eneo hilo. Wakati huohuo Sector East ilipewa Jeshi la Polisi la Indonesia.