Operation title

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea na majukumu ya Ulinzi wa Amani sehemu mbalimbali zenye migogoro ndani na nje ya Bara la Afrika chini ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.. Pamoja na vikundi vya Ulinzi wa Amani JWTZ vilevile limetoa Maafisa na Askari kama waangalizi wa Amani (MILOBS) na wanadhimu (SO) katika misheni mbalimbali.

Africa Union - United Nations Mission in Darfur

JWTZ linaendelea kushiriki katika misheni hii tangu 2008 kwa kutumia kikosi kimoja chenye watu 800 kinachobadilishana kila mwaka mmoja. Kikosi hiki hujulikana kama TANZBATT - 1 hadi TANZBATT - 10