Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea na majukumu ya Ulinzi wa Amani sehemu mbalimbali zenye migogoro ndani na nje ya Bara la Afrika chini ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.. Pamoja na vikundi vya Ulinzi wa Amani JWTZ vilevile limetoa Maafisa na Askari kama waangalizi wa Amani (MILOBS) na wanadhimu (SO) katika misheni mbalimbali.
United Nations Stabilization Mission in the Democratic Republic of Congo
JWTZ lilipeleka kikosi cha kwanza chenye wanajeshi 1256 kwenye misheni hii mwaka 2013 na linaendelea kushiriki hadi sasa. Kikosi hiki kinajulikana kama TANZBATT - 1 DRC hadi TANZBATT - 3 DRC ambayo inaendelea na majukumu nchini humo.