Kamandi ya MMJ
Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi
Kuanzishwa kwa Kamandi
Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi ni Kamandi mpya ambayo uanzishwaji wake ulianza rasmi baada ya kikao kilichofanyika chini ya Halmashauri ya Majeshi ya Ulinzi kwa kupitisha uamuzi wa kuanzishwa kwake mwaka 2013.
Kamandi ilianza kama GOC kwa kufuata mtiririko maalum hadi kufikia Kamandi kamili. Tangu Kamandi ianzishwe iliongozwa na Makamanda wafuatao:
- Meja Jenerali HV Chema kuanzia tarehe 01 Jul 14 hadi 28 Sep 14
- Brigedia Jenerali JK Mrema kuanzia tarehe 06 Jun 11 hadi 30 Jun 14
- Brigedia Jenerali DB Mrope kuanzia tarehe 29 Sep 14 hadi 15 Sep 15
- Meja Jenerali IS Nassor kuanzia tarehe 16 Sep 15 hadi 18 Feb 16
- Brigedia Jenerali DB Mrope kuanzia tarehe 19 Feb 16 hadi 9 Jul 17
- Meja Jenerali SS Othman kuanzia tarehe 15 Feb 18 hadi 30 Jun 20.
- Brigedia Jenerali RG Mwaisaka kuanzia tarehe 01 Jul 20 hadi 11 Jun 21, baada ya kupandishwa cheo kipya kuwa Meja Jenerali aliteuliwa kuendelea kuongoza Kamandi hiyo hadi tarehe 01 Feb 22.
- Brigedia Jenerali IS Nkambi kuanzia tarehe 01 Feb 22 hadi 28 Jul 22, baada ya kupandishwa cheo kipya kuwa Meja Jenerali aliteuliwa kuendelea kuongoza Kamandi hiyo hadi hivi sasa.
Majukumu ya Kamandi
- Kushughulika na utawala na uendeshaji wa vikosi na shule zilizopo chini ya Makao Makuu ya Jeshi
- Kuhakikisha maelekezo yanayotolewa na Makao Makuu ya Jeshi yanawafikia walengwa na yanatekelezwa.
- Kusimamia mafunzo na utayari kivita wa vikosi ni wa hali ya juu wakati wote
- Kuhakikisha zana na vifaa vinakuwa katika hali nzuri kiutendaji