Strategic Intelligence, Washington DC
Jenerali Venance Mabeyo ni Mkuu wa Majeshi wa nane kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tangu alipoteuliwa tarehe 06 February 2017 na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli.
Jenerali Venance Mabeyo alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 January 1979 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1980 kuwa Luteni Usu.
Jenerali Venance Mabeyo alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadhi ya nchi hizo ni Kenya, India, Canada na Marekani
Jenerali Venance Mabeyo katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwambata Jeshi nchini Rwanda, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi , Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.
Jenerali Venance Mabeyo ametunukiwa medali mbalimbali
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.