• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Askari Wapya JWTZ wahitimu mafunzo

Askari Wapya JWTZ wahitimu mafunzo Posted On: Saturday, 31st January 2026

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amefunga rasmi Mafunzo ya Askari wapya katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS) Kihangaiko Msata Mkoani Pwani leo tarehe 31 Januari 2025.

Jenerali Mkunda amewataka askari wapya kukiishi na kuzingatia kiapo cha utii wakati wote watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao sehemu mbalimbali watakayopangiwa, huku akisisitiza kuchukuliwa hatua kwa askari watakaokwenda kinyume na kiapo chao.

Askari wapya wameaswa kutotenda mambo ambayo ni kinyume na taratibu za kijeshi ikiwemo kutojihusisha na siasa, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, matumizi ya madawa ya kulevya, michezo ya kamari na kuepuka madeni yasiyo na tija.

Mkuu wa Majeshi amewataka Askari hao kutunza Afya zao na kuzingatia lishe bora wakati wote wanapotekeleza majukumu yao. Aidha, wasijihusisha na uhalifu wa aina yoyote kwani watakuwa wamekwenda kinyume na sheria na taratibu za kijeshi hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Jenerali Mkunda amesisitiza Askari hao kuwa tayari kiakili na kisaikolojia kuitetea nchi kwa kutekeleza majukumu ya Jeshi ndani na nje ya Tanzania.

Naye, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Kihangaiko Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myala ametoa pongezi kwa Askari wapya waliohitimu mafunzo na kuwa tayari kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Brigedia Jenerali Myala amesema Askari wapya wapo tayari kutekeleza majukumu mbalimbali ya kijeshi kutokana na mafunzo waliyoyapata. Shule ya RTS Kihangaiko itaendelea kushirikiana na Makao Makuu ya Jeshi kuboresha mazingira ya Mafunzo ili kuendelea kuwafunza vijana kuwa askari Hodariwatakaokuwa na uwezo wa kushiriki katika ulinzi ndani na nje ya nchi.

Askari wapya Kundi la 44/25 waliohitimu mafunzo wapo tayari kushiriki katika majukumu ya ulinzi wa taifa hasa katika mipaka ya nchi na kutambua majukumu yao mengine yakiwemo kumtii na kumlinda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuuna kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari Mpya

  • Askari Wapya JWTZ wahitimu mafunzo

    Askari Wapya JWTZ wahitimu mafunzo

    tokea masaa 11
  • Waziri Atembelea Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

    Waziri Atembelea Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

    tokea wiki 1
  • Meja Jenerali Gaguti Afunga rasmi zoezi la Medani Msata

    Meja Jenerali Gaguti Afunga rasmi zoezi la Medani Msata

    tokea wiki 2
  • Rais Samia afungua Mkutano wa CDF na Makamanda JWTZ

    Rais Samia afungua Mkutano wa CDF na Makamanda JWTZ

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 9
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 9
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 9
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 3
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.