Posted On: Thursday, 12th February 2026
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda leo tarehe 12 Februari 2026 ameweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Jengo la utawala katika Kamandi ya Jeshi la Akiba iliyopo Mkoani Singida.
Akizungumza na Maafisa na Askari wa Kamandi hiyo, Jenerali Mkunda alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha JWTZ kwa kutoa rasilimali fedha pamoja na vifaa ili kuhakikisha kuwa Jeshi linatekeleza majukumu yake ya kiulinzi na usalama nchini.
Aidha aliwataka wanakamandi ya Jeshi la Akiba kuhakikisha Ujenzi huo unaisha kwa wakati pamoja na kutunza miundombinu ya Jengo hilo pindi litakapoanza kutumika.
Pia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mkunda aliwashukuru wanakamandi kwa jitihada kubwa walizofanya kuhakikisha Ujenzi huo unaanza kwa wakati hadi kufikia hatua iliyopo na kuwasihi kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano na jamii inayowazunguka huku akisisitiza kutunza afya zao kwani wao ndiyo nguvukazi ya taifa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.