Posted On: Friday, 5th June 2026
Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Idd Said Nkambi, amefungua kikao kazi cha Polisi Jeshi kinachofanyika katika Kikosi cha Mazao Mkoani Morogoro leo tarehe 04Jun26.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Meja Jenerali Nkambi amewaasa Polisi Jeshi kujadili kwa weledi mambo ya Msingi hasa katika kufanya maamuzi ya utoaji haki kwa kuzingatia kipindi hiki cha mabadiriko ya sayansi na teknolojia.
Kikao kazi hiki kinachoongozwa na Mkurugenzi wa Polisi Jeshi Brigedia Jenerali Abubakar Charo ni mwendelezo wa vikao vinavyofanyika kila mwaka katika kamandi mbalimbali ambapo sasa ni zamu ya Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi huku kikiwa ni kikao cha Saba.
Washiriki wa Kikao ni Maafisa wanadhimu kutoka Kurugenzi ya Polisi Jeshi Makao Makuu ya Jeshi, Kurugenzi ya Polisi Jeshi Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, Wakuu wa Polisi Jeshi wa Kamandi, na Brigedi na shule za Mafunzo ya Kijeshi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.