• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Luteni Jenerali Othman aweka jiwe la msingi kuzindua Miradi ya Ujenzi Kisarawe

Luteni Jenerali Othman aweka jiwe la msingi kuzindua Miradi ya Ujenzi Kisarawe Posted On: Tuesday, 9th June 2026

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman ameweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Kijiji cha burudani kilichopo katika Kambi ya Jeshi Kisarawe Mkoani Pwani leo tarehe 08 Juni 26.

Akizungumza na Maafisa na Askari wa Kikosi cha mawasiliano Kisarawe, Luteni Jenerali Othman amesema kuanzishwa kwa miradi hii kutasaidia kikosi kutatua changamoto za mbalimbalii.

Miradi iliyoanzishwa ni pamoja na Ujenzi wa uwanja wa michezo, maegesho ya magari ya mizigo, Ujenzi wa Ukumbi wa Burudani na Ujenzi wa kituo cha mafuta.

Aidha, Luteni Jenerali Othman amewataka wanakikosi kuepuka tabia zisizofaa ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, matumizi mabaya ya mitandao ya Kijamii, uraibu wa kushiriki michezo ya kubashiri na ulevi uliokithiri.

Pia, wanakikosi wametakiwa kuyaishi maneno manne kwa mwanajeshi ikiwemo nidhamu nzuri, Utii, Uhodari na Uaminifu, maneno ambayo hayana budi kuzingatiwa wakati wote.

Naye, Kamanda Kikosi cha mawasiliano Kisarawe Kanali Mwakisamba amemshukuru Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Salum Haji Othman kwa kuweka jiwe la msingi kujengwa kwa miradi ya kikosi, na kuahidi kukamilisha miradi hiyo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na maafisa Jenerali na Wakuu wa Vikosi kutoka Kanda ya Pwani na Dar es Salaam pamoja na Wanakikosi.

Habari Mpya

  • Luteni Jenerali Othman aweka jiwe la msingi kuzindua Miradi ya Ujenzi Kisarawe

    Luteni Jenerali Othman aweka jiwe la msingi kuzindua Miradi ya Ujenzi Kisarawe

    tokea masaa 11
  • Kikao cha Polisi Jeshi chafunguliwa Morogoro

    Kikao cha Polisi Jeshi chafunguliwa Morogoro

    tokea siku 4
  • Rais azindua jengo la MMUT

    Rais azindua jengo la MMUT

    tokea miezi 3
  • Jenerali Mkunda Aweka Jiwe la Msingi Jeshi la Akiba

    Jenerali Mkunda Aweka Jiwe la Msingi Jeshi la Akiba

    tokea miezi 3
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 9
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 9
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 9
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 3
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.