• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Meja Jenerali Gaguti Afunga rasmi zoezi la Medani Msata

Meja Jenerali Gaguti Afunga rasmi zoezi la Medani Msata Posted On: Saturday, 17th January 2026

Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Marco Gaguti amefunga rasmi zoezi la Medani la EX- MALIZA lililofanywa na Kuruti wa Kundi la 44/25 katika eneo la Msata tarehe 16 Januari 2026.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Meja Jenerali Gaguti amewataka Kuruti hao wanaotarajia kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi hivi karibuni kuwa waadilifu, kujituma na kuwa watiifu kwa nchi yao.

Kuruti walioshiriki zoezi, wametakiwa kuzingatia mafunzo ya nadharia na vitendo kama shambulio la kunuia, shambulio la kushtukiza na somo la doria huku akionyesha wazi kuwa zoezi limefanikiwa. Dhamira ya Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ni kuona kuruti wote wanahitimu na kwenda katika maeneo mbalimbali watakayopangiwa kushiriki kulilinda taifa.

Meja Jenerali Gaguti aliongeza kuwa Mafunzo na Mazoezi mbalimbali ya medani ndio msingi wa JWTZ kwani Jeshi imara linatokana na uwepo wa mazoezi ya medani.

Kuruti wanaotarajiwa kuhitimu kozi ya mafunzo ya awali wamesisitizwa kuzingatia mambo makuu manne kwa mwanajeshi ambayo ni Nidhamu nzuri, Uhodari, Utii na Uaminifu ambayo yamewajenga wanajeshi na kutekeleza majukumu kwa weledi.

Naye, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myalla amesema kuwa wanafunzi wa kozi ya mafunzo ya awali wameonyesha uwezo wa kukabiliana na adui kwa kulifanya zoezi kuwa na mafanikio makubwa.

Brigedia Jenerali Myalla amesema kuwa zoezi limewajenga kuruti kuwa na uzalendo, kudumisha mahusiano na raia, kuwajengea uwezo wa kufanya operesheni katika mazingira yoyote ndani na nje ya nchi.

Kuruti wamejengewa ujasiri na kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika mazingira ya medani.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kufanikisha kufanyika mazoezi mbalimbali ya medani kwa Kozi za Mafunzo ya Awali katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko ili kuwajengea uwezo askari wapya, namna ya kuilinda nchi ya Tanzania kwa kushirikiana na wananchi.

Habari Mpya

  • Meja Jenerali Gaguti Afunga rasmi zoezi la Medani Msata

    Meja Jenerali Gaguti Afunga rasmi zoezi la Medani Msata

    tokea masaa 4
  • Rais Samia afungua Mkutano wa CDF na Makamanda JWTZ

    Rais Samia afungua Mkutano wa CDF na Makamanda JWTZ

    tokea mwezi 1
  • Dr Nyamsaho atembelea Makao Makuu ya Jeshi

    Dr Nyamsaho atembelea Makao Makuu ya Jeshi

    tokea mwezi 1
  • Rais Samia atunuku Kamisheni

    Rais Samia atunuku Kamisheni

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 9
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 9
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 9
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 3
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.