Posted On: Monday, 15th December 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Mkutano wa 09 wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania unaofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga iliyopo Mkoani Tanga leo tarehe 15 Disemba 2025.
Akizungumza na Makamanda, Mheshimiwa Rais amelipongeza JWTZ kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa kwa kuhakikisha Taifa liko salama wakati wote. Amewahakikishia Makamanda kuwa Serikali itaendelea kuliwezesha JWTZ kwenye kila Nyanja ikiwemo zana, vifaa, Miundombinu na Mafunzo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa utulivu.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa namna Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuliwezesha JWTZ kutekeleza majukumu yake. Amemhakikishia kuwa Jeshi litaendelea kulinda mipaka ya nchi na watu wake dhidi ya matishio yoyote yatakayojitokeza .
Mkutano wa CDF na Makamanda wa JWTZ ni jukwaa lililoanzishwa na Mkuu wa Majeshi likiwa na lengo la kuwakutanisha Makamanda ili kupata wasaa wa kujadiliana maswala mbalimbali ya Ulinzi kwa maslahi ya Taifa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.