Master in Security and Strategic Studies
Luteni Jenerali Mathew Mkingule ni Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa 14 tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 21 Agosti, 2021.
Luteni Jenerali Mathew Mkingule alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 21 Februari, 1995 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1995 kuwa Luteni Usu.
Luteni Jenerali Mathew Mkingule alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya.
Katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Mathew Mkingule alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Naibu Mkurugenzi wa Bajeti na Usimamizi wa Fedha, Mkurugenzi wa Fedha za Umma na Hesabu, Mkurugenzi wa Bajeti na Usimamizi wa Fedha na baadae kuwa Mdhibiti Mkuu wa Fedha Makao Makuu ya Jeshi.
Luteni Jenerali Mathew Mkingule ametunukiwa medali mbalimbali
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.