Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stagomena Tax leo tarehe 18 Juni 2022 ametunuku Stashahada na Shahada ya Uzamili ya Mafunzo ya Ulinzi na Usalama kwa jumla ya Maafisa 67waliokua katika Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duluti Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Wahitimu 16 wametunukiwa Stashahada ya Mafunzo ya Ulinzi na Usalama, huku wengine 51 wakitunukiwa Shahada ya Uzamili ya Mafunzo ya Ulinzi na Usalama.
Awali, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Brigedia Jenerali Sylivester Ghuliku aliwatunuku Wahitimu wote 67 Beji ya Ukamanda na Unadhimu Kundi la 36/21 na kuonyesha kuwa Maafisa wamemaliza Kozi hiyo yenye tija katika utendaji Kijeshi.
Akizungumza mara baada ya kutunuku Stashahada na Shahada ya Uzamili katika mafunzo ya Ulinzi na Usalama, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, amewataka Wahitimu wakaitumie elimu hiyo kutatua changamoto mbalimbali za kiusalama ikiwemo namna ya kukabiliana na matishio ya Ugaidi duniani ambayo yamekua yakisumbua kwa sasa. Pia, amesisitiza kuwa wahitimu kutoka nje wakawe mabolozi Wazuri kutokana na kila walichokipata Tanzania, na kuongeza kuwa Ulinzi na Usalama haunabudi kuimarishwa katika Jumuiya za Kikanda.
Kozi hiyo ilijumuisha Maafisa kutoka Nchi mbambali kama Bangladesh, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Eswatini, Kenya, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Rwanda na Uganda.
Elimu walioipata Wahitimu itasaidia Majeshi ya Nchi hizo kukabiliana na changamoto za Kiulinzi, kwani kuimarika kwa Ulinzi kutasababisha Nchi kuendelea na shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wa Nchi mbalimbali zikiwemo Jumuiya za Kikanda.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.