Mkuu wa Tawi la Utumishi Jeshini Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti amefunga Mafunzo ya Awali ya Kijeshi kwa Askari wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi Kihangaiko kwa Gwaride rasmi.
Meja Jenerali Gaguti aliambatana na Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Wanadhimu kutoka Makao Makuu ya Jeshi, Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Dini.
Kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Meja Jenerali Gaguti aliwaasa Askari wapya kuishi kwa kuzingatia viapo vyao vya utii, kutunza afya zao na kusisitiza kuwa tayari kuilinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sherehe za ufungwaji wa kozi hiyo zimepambwa na maonesho mbalimbali ya utendaji kivita kama kupambana na adui, kuruka vikwazo, karate, matumizi ya silaha pamoja na kufanya doria.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.