Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA), limesema kuwa michezo ya majeshi Tanzania itaanza kutimua vumbi tarehe 23 mwezi huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Upanga jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Baraza hilo Brigedia Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa jumla ya Kanda saba zitashiriki katika Michezo hiyo.
Kwa mwaka huu michezo ya BAMMATA inashirikisha kanda saba (7) ambapo timuza michezo mbalimbali zinatoka ndani ya kanda hizo. Kanda zinazoshiriki mwaka huu ni Ngome, JKT, Polisi, Magereza, SMZ (Idara Maalumu), Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 9203 Dar es Salaam,
Street :Magore, Upanga
Fax : +255 22 2153432
Tel : +255 22 2150592- 4
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.