Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na MichezoMhe.Dkt. Harisson Mwakyembe (MB), tarehe 18 May 2018 amefungua rasmi mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP) 2018 katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika ufunguzi huo Mhe. Waziri aliongea na hadhira iliofika uwanjani hapo na kuwataka wapiganajiwarudishe hadhi iliyokuwepo miaka ya nyuma,. Mfano, kipindi cha akina Filbert Bayi, Juma Ikang’aa na wengine wengi ambao waliiletea sifa Taifa letu.
Lengo la Mashindano hayo ni kuvumbua vipaji na kupata timu ya Jeshi itakayoshiriki katika michezo ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Janerali Yakubu Mohamed alimuhakikishia Mgeni Rasmi kuwa Tanzania itafanya vizuri katika mashindano hayo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.