Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ‘CDF CUP’ 2018 yamefungwa rasmi leo Mei 18, 2018 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo.
Jenerali Mabeyo amewapongeza washiriki wote kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu tangu mashindano yalipoanza, na pia kuwataka kuendelea na nidhamu hiyo watakapokuwa kambini wakijiandaa na Michezo ya Majeshi kwa Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani nchini Kenya.
Sherehe za ufungaji wa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ‘CDF CUP’ 2018 zilitanguliwa na fainali ya mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) dhidi ya Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi (Ngome), ambapo JKT waliibuka washindi kwa kuifunga ngome 1 : 0 .
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.