Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na Majeshi ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki limeendelea kutoa misaada ya dawa na vifaa tiba pamoja na vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali na makundi yenye uhitaji maalum kisiwani Unguja Zanzibar.
Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Ushirikiano baina ya raia na Majeshi (CIMIC) wa JWTZ Brigedia Jenerali Daktari Agatha Mary Katua.
Akizungumza mara baada ya kutoa misaada hiyo Brigedia Jenerali Daktari Katua ambaye pia ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kuwa JWTZ ni Jeshi lao na liko kwa ajili yao.
Amesema kuwa huu ni mwanzo tu wa ushirikiano kati ya Jeshi na wananchi lakini wategemee ushirikiano mkubwa zaidi.
Utoaji wa misaada hiyo ni muendelezo wa wiki ya ushirikiano kati ya Jeshi na wananchi kutoka Majeshi ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na kilele chake ni tarehe mosi Septemba siku ambayo ni siku ya Majeshi (JWTZ).Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.