Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Hafla hiyo imefanyika tarehe 02, Novemba 2020 katika uwanja wa Amani mjini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu.
Akizungumza baada ya kuapishwa Dkt Hussein Mwinyi amewataka Wazanzibari kuachana na tofauti zao ili washirikiane kujenga Zanzibar mpya.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.