Posted On: Friday, 5th December 2025
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Rhimo Nyamsaho amefanya ziara fupi Makao Makuu ya Jeshi Msalato Dodoma leo tarehe 05 Desemba 2025 kwa lengo la kujitambulisha.
Baada kupokelewa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda, Dkt Rhimo Nyamsaho alizungumza na Maafisa na Askari akiwaasa kudumisha umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Alisisitiza suala zima la kutanguliza maslahi ya Taifa ili kuhakikisha suala la Ulinzi wa Taifa linaimarika kwa kiwango cha juu.
Mhe. Waziri aliwataka Maafisa na Askari kudumisha sifa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tangu kuasisiwa kwake kwa kuendelea kuviishi viapo vyao ikiwemo Nidhamu nzuri, Utii, Uhodari na Uaminifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amempongeza Mheshimiwa Dkt Nyamsaho kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT na kumuhakikishia kuwa JWTZ liko imara na tayari wakati wote kutekeleza majukumu yake kwa nidhamu na uadilifu wa hali ya juu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.