Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo March 3, 2022 limekabidhiwa Jengo la Utafiti na Kikundi cha Ushauri wa Kiufundi Cha Jeshi la Ujerumani (German Armed Forces Technical Advisory Group - GAFTAG) lililojengwa katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam. Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti (United National Institute of Training and Research – UNITAR).
Makabidhiano hayo yamefanyika kati ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Mathew Mkingule ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti Claudia Cnoci ambaye amemuwakilisha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Kathrin Steinbrenner.
Kupatikana kwa Jengo hilo kutasaidia kuboresha mafunzo na utafiti katika Kituo Cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani. Aidha, Maafisa na Askari watakaopata mafunzo kituoni hapo watanufaika kwa kupata ujuzi zaidi kabla ya kwenda kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani watakapopangiwa. Vile vile mafunzo hayo yatawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi na weledi.Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.