Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetimiza miaka hamsini na tano (55) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964. Sherehe hizi hufanyika kila mwaka baada JWTZ kuchukua nafasi ya Jeshi lililokuwa limeanzishwa na Mkoloni likiitwa Tanganyika Riffle.
Akizungumza katika sherehe hizo mgeni rasmi Brigedia Jenerali Justus Stephen Mnkande alisema Jeshi ni chombo muhimu hasa katika maslahi ya nchi akitolea mfano kulinda mipaka ya nchi, kushiriki kwenye Ulinzi wa amani pamoja na kushiriki kwenye shughuli za kijamii.
Sherehe hizi zilijumuisha vikundi mbalimbali vya burudani vikiwemo vikundi vya ngoma, mchezo wa mpira wa miguu na sarakasi ikiwa kama desturi ya kudumisha na kuimarisha Umoja wa JWTZ.
Akihitimisha sherehe hizi zilizofanyika Mwenge kwenye Viwanja vya Vinyago Brigedia Jenerali Mnkande aliwasihi maafisa, askari na raia waliohudhuria kwenye sherehe hizi kuzidi kuweka uzalendo wa Taifa letu mbele ili kuendelea kuimarisha amani ya Taifa letu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.