Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amefanya ziara mkoani Ruvuma na Lindi kwa kuyatembelea maghala makuu yaliotengwa na Serikali kwa ajili ya kuhifadhia Korosho katika zoezi la Operesheni Korosho linaloendelea nchini. Aidha Jenerali Mabeyo aliwatembelea wajasiriamali wadogo wanaobangua na kuuza korosho.
Jenerali Mabeyo alianza ziara kwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Homela ambapo alipewa taarifa ya zoezi hilo pamoja na hali ya ulinzi na usalama wilayani hapo.
Mhe. Homela amelipongeza Jeshi kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea nao katika kufanikisha jukumu la ukusanyaji korosho kwa uadilifu mkubwa kwa kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kama Serikali ilivyoagiza.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.