Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amekutana na Maafisa Wakuu na Maafisa Wadogo wa Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) tarehe 20 Aprili, 2018 wakati wa 'Happy hour' iliyofanyika katika bwalo la Maafisa Upanga jijini Dar es salaam.
“ Happy Hour” ni hafla fupi ambapo Mkuu wa sehemu husika hutumia fursa hiyo kukaa pamoja na Wafuasi wake na hukumbusha mambo mbalimbali ya kijeshi yanayoonekana hayaendi vizuri na kuwataka maafisa kuishi maisha ya kijeshi badala ya kuishi kwa tamaduni ambazo si za kijeshi.
Wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Majeshi amewataka Maafisa kudumisha mila, desturi na utamaduni wa Jeshi kwa kukutana na kupata huduma katika mabwalo ya Jeshi hilo.
Vilevile Jenerali Mabeyo amewataka Maafisa kudumisha nidhamu wakiwa katika majukumu yao ya kila siku.
Aidha, Maafisa hao walibadilishana mawazo na uzoefu mbalimbali wakati wa hafla hiyo
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.