Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Salvatory Mabeyo leo tarehe 26 Februari 2020 amezindua rasmi Makao Makuu Mapya ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyopo wilaya ya Chamwino mjini Dodoma
Aidha Jenerali Mabeyo ameipongeza JKT kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya ujenzi waliyopewa na serikali kwa kufanya vizuri na kusisitiza waendelee kufanya vizuri zaidi. Hatua hiyo ni baada ya serikali kuwaamini na kuwatumia kutekeleza miradi ya Taifa kufikia uchumi wa kati ikiwa ndio kaulimbiu ya serikali ya awamu ya tano
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na Maafisa, Askari, Watumishi wa umma na Wananchi wa maeneo hayo
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 9203 Dar es Salaam,
Street :Magore, Upanga
Fax : +255 22 2153432
Tel : +255 22 2150592- 4
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.