Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda alipokwenda kumtembelea Ikulu ya Zanzibar tarehe 14 Julai 2022.
Katika mazungumzo yao Rais Mwinyi amempongeza Jenerali Mkunda kwa kuteuliwa kuliongoza Jeshi, na akamtakia heri katika kutekeleza majukumu yake mapya. Rais Mwinyi aliongeza kwa kusema anaamini Jeshi liko kwenye mikono salama kwani anafahamu uwezo alionao Jenerali Mkunda.
Naye Jenerali Mkunda amemshukuru Rais Mwinyi kwa nasaha zake, na akasema Jeshi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuendelea kuifanya Tanzania kuwa na amani na utulivu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.