Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amefanya ziara na kutembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi inayojengwa Msalato Jijini Dodoma.
Jenerali Mkunda akiwa ameambatana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Wakuu wa Kamandi na Matawi wa Makao Makuu ya Jeshi amepongeza maendeleo makubwa ya mradi huo yaliyofikiwa.
Naye Meneja wa Mradi huo Bi. Jackline Benson amesema kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ya Daraja la Nne kwa ngazi ya Kimataifa umefikia asilimia 80 ya ujenzi huo.
Hospitali hiyo ikikamilika itatumika kuwahudumia wanajeshi pamoja na wananchi wote kwa ujumla.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.