Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan amewasilisha Salamu za rambirambi kwa familia za wapiganaji wawili Sgt Mohammed Abdallah Suleiman na Pte John Nyewata John waliofariki kwa kushambuliwa na Kikundi cha Waasi cha M23 mwezi Januari 2025 mjini Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wanafamilia, ndugu na wanahabari nyumbani kwa wazazi wa marehemu eneo la Kiembe Samaki Zanzibar na Kishiri Jijini Mwanza Jenerali Mkunda amesema Mashujaa hao walipoteza maisha wakitekeleza jukumu la Ulinzi wa amani chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC.
Amewaambia ndugu na jamaa wa marehemu kuwa Mheshimiwa Rais amesikitishwa sana na vifo vya Mashujaa wetu na anaungana nao katika kuomboleza vifo vya wapendwa wao.
Sambamba na Salamu za rambirambi, Mheshimiwa Rais ametoa ubani kwa familia hizo ikiwa ni pole kwa msiba huo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.