Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewataka Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Vyombo vya Usalama pamoja na Watumishi kutoka Taasisi za Serikali watakaoshiriki Zoezi la Ushirikiano Imara 2024, kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi wakati wa kukabidhi bendera ya Tanzania kwa Vikundi vinavyoshiriki Zoezi hilo, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Meja Jenerali Fadhil Omary Nondo amesema kuwa mazoezi ya pamoja kwa vikundi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki yanalenga kujenga uwezo wa pamoja na utayari katika kukabiliana na Ugaidi, Majanga ya asili,Uharamia na Ulinzi wa Amani.
Zoezi la Ushirikiano Imara linashirikisha vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na watumishi kutoka Taasisi na Idara mbalimbali za serikali kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zoezi la Ushirikiano Imara 2024 linatarajiwa kufanyika nchini Rwanda kuanzia tarehe 08 Juni mwaka huu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.